MAJONZI TELE: Shuhudia Waziri KOMBANI Alivyoagwa Leo Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar!



Makamu wa Rais, Dk. Bilal akielekea kutoa heshima za mwisho kwa Kombani. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar Balozi, Seif Ally Idd, akitoa heshima za mwisho. Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akiuaga mwili wa marehemu Kombani. Anne Makinda akitoa heshima za mwisho kuaga mwili wa Celina Kombani. Mama Maria Nyerere akiwa mbele ya jeneza. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva, akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza.



Kamanda Maalum wa Kanda ya kipolisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova naye alikuwepo. Huyu ni Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Fenala Mkangala. Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipita mbele ya jeneza. 
Hapa ni Waziri wa Uchukuzi, Samweli Sitta akionyesha masikitiko yake. Anne Makinda (katikati) akiwa na Mama Maria Nyerere (kushoto) katika viwanja vya Karimjee kabla ya kuuaga mwili wa Kombani. Gari lililokuwa limebeba mwili wa marehemui.Jeneza la mwili wa Kombani likiwa katika viwanja vya Karimjee. Msanii wa filamu Wema Sepetu akiuaga mwili wa Kombani. Waombolezaji wakielekea kwenye jeneza.


Hali ilivyokuwa viwanjani hapo. Mmoja wa wanafamilia akilia kwa uchungu. Mume wa marehemu Kombani (katikati) akiwa na simanzi.Celina Kombani enzi za uhai wake.
ALIYEKUWA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani, ameagwa leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na viongozi wa serikali, kada na rika mbalimbali, ambapo mwili umesafirishwa kwenda kijijini kwake, Mahenge – Ulanga mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viwanjani hapo ambapo mwili wake umeagwa, baadhi ya wanachama wa CCM, wakiwemo mawaziri na viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama na serikali, wamemwelezea Bi. Kombani kama mmoja wa viongozi walioacha alama iliyotukuka katika ngazi ya utumishi, kulingana na weledi na uwezo wake wa kiutendaji.

Katika salamu zake kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekuwa spika, Bi. Anne Makinda amesema uwezo wa Kombani ulisaidia kutatua baadhi ya mambo ya kiutawala ndani ya bunge huku akieleza kwa hisia kali namna alivyoguswa na msiba huo mzito kwa taifa.
“Hakika alikuwa na uwezo wa kipekee, hivi karibuni siku chache kabla ya kifo chake, tulikutana hapa jijini Dar kwa ajili ya kumuomba ushauri wake kwenye mpango wa kukuza muundo wa bunge ambapo, alitoa mchango wake vizuri, taifa limepoteza nguvu kazi muhimu sana,” alisema Bi. Makinda.

Marehemu Celina Kombani alifariki dunia Septemba 24 mwaka, katika Hospitali ya Appollo nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibahu ya ugonjwa wa kansa.
Kabla ya wadhifa wake wa sasa ndani ya utumishi, Kombani aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi) 2008-2010, Waziri wa Katiba na Sheria, Naibu Waziri Tamisemi, Ofisa Utawala mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Meneja wa Kiwanda cha ngozi Morogoro na ofisa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Bwana alitoa, Bwana ametwa jina lake lihimidiwe. Amen!

PICHA/STORI: DENIS MTIMA NA BRIGHTON MASALU/GPL
MAJONZI TELE: Shuhudia Waziri KOMBANI Alivyoagwa Leo Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar! MAJONZI TELE: Shuhudia Waziri KOMBANI Alivyoagwa Leo Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar! Reviewed by Jason on 22:05 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.